Drama ndani ya familia ya Zulu yazidi kupamba moto! Mqhele anakutana na kikao cha kaka zake na kuulizwa kama kweli amempiga mkewe. Anakiri makosa yake na anadhibiwa vikali. Wakati huo huo, Ngoba anajivunia mbele ya kaka zake kuhusu mahusiano yake ya siri na mke wa Kamishna — uhusiano uliowawezesha kufanikisha tukio la uporaji wa kasino. Lakini bila kujua, mpenzi wake Mandisa anasikiliza kwa hasira kali… na uamuzi wake ni wa kushangaza: anachoma hela hizo wakati tayari wamemuita Kamishna aje kuchukua sehemu yake. Je, familia hii itaweza kupona baada ya usaliti huu mkubwa? Usikose The Wife kwenye Maisha Magic Bongo!