Tukiwa katika msimu huu wa mvua, mtindo wa maisha yetu yanabadilika. Huu ndio wakati wa watu kukimbizana kutoa miamvuli yao ndani na kwa wakazi wa Dar es Salaam tunaona hata masweta na makoti nayo yakitolewa.
Nyakati kama hizi, hakuna njia bora ya kujiliwaza zaidi ya kujiachia katika ulimwengu wa tamthilia na filamu za kusisimua, na Maisha Magic Bongo inahakikisha hukosi kupata burudani hiyo kwa kukuletea vipindi vikali.
Ukiwa ni mpenzi wa simulizi za mapenzi, maisha ya vijana wa mjini na changamoto zao, au filamu zinazokufanya uangalie kwa mshangao mkubwa, yote hayo unayapata ndani ya Maisha Magic Bongo. Itakapoanza kunyesha jilaze sebuleni na kikombe chako cha chai ya moto na ufurahie drama zinazobeba hisia kali- kutoka kwenye mapenzi yakuvutia, vichekesho, hadi maisha halisi yanayogusa mioyo yetu.
Na katika mwezi huu wa April, Maisha Magic Bongo inaingia kwenye msimu wa mwisho wa tamthilia mbili za kuumiza moyo: Gharika na Yolanda. Mambo yanazidi kuwa magumu, na hakuna anayetaka kukosa kuona hatima ya wahusika hawa waliokonga nyoyo za wengi.
Katika Gharika, familia hupambana na matokeo ya maamuzi magumu, wakati usaliti, tamaa na upendo vina jukumu kubwa. Hakuna anayeweza kutabiri mwisho utakuwaje - je, haki itapatikana au wahusika wetu watajikuta wakizama katika mafuriko ya hatima zao wenyewe?
Wakati huo huo, huko Yolanda, maisha ya msichana anayejitahidi kujikomboa kutoka kwa maisha magumu na mateso mambo yanazidi kuwa magumu. Ndoto zake zinakaribia kufa, lakini, je njama zinazomzunguka zinaweza kubadilisha kabisa hatima yake? Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona kama atafanikiwa au kama mwisho wake utakuwa ni wa kusikitisha.
Kuna ladha ya kipekee katika kutazama tamthilia wakati mvua inanyesha. Unapokunywa kikombe cha chai ya moto na huku unangalia wasanii wako unaowapenda wanapokabiliana na ngumu, unatekwa kabisa na kuanza kuhisi na wewe kama uko ndani za hadithi zao za kusimumua. Kuna wakati unajikuta unacheka peke yako, wakati mwingine unashtuka kwa mshangao, na wakati mwingine hata machozi yanataka kukutoka bila kutarajia. Hii ndio burudani ya kweli inayokufanya usahau hata kama kuna mvua ya nje.
Tulia zako ndani, jifunike vizuri, tafuta vitafunwa na washa Maisha Magic Bongo DStv Channel 160. Nje kuna mvua na kibaridi flani, lakini ndani kuna hadithi za joto zinazokupa burudani isiyo na kifani.